Kulipa Kodi share
Mamlaka ya Mapato Tanzania ina jukumu la kukusanya kodi nyingi nchini Tanzania. Mamlaka za Serikali za Mitaa pia zina mamlaka ya kukusanya baadhi ya kodi na tozo. Kodi zinaweza kuwa za moja kwa moja au zisiwe za moja kwa moja. Kodi za moja kwa moja hasa zinahusu kodi ya mapato wakati kodi zisizo za moja kwa moja zinahusu biashara ya kimataifa na ya mlaji. Njia za malipo ya kodi ni kwa zuio, kulipa kwa awamu na makadirio. Kwa kawaida kila mtu anatakiwa kulipa kodi kwa awamu na kwa makadirio. Njia ya zuio ipo tu kwa wale wanaotakiwa kuzuia kodi ambao ni :
- Waajiri wanaofanya malipo yatakayojumuishwa katika kukokotoa mapato yanayostahili kutozwa kodi ya mtumishi kutokana na ajira;
- Watu wanaolipa mapato ya uwekezaji (k.m. wale wanaolipa gawio, riba, malipo ya maliasili, kodi au mrabaha);
- Watu wanaolipa ada ya huduma na malipo ya mkataba. Hata hivyo kuna yasiofuata utaratibu huo. Usajili wa kodi hufanywa katika vituo vya kodi vya TRA karibu na eneo lako la biashara. Kodi pia zinalipwa kupitia benki;
➢ Usajili wa kodi hufanywa katika vituo vya kodi vya TRA karibu na eneo lako la biashara. Kodi pia zinalipwa kupitia benki. Bofya h apa kupata orodha ya ofisi za mkoa za TRA.