Huduma kwa wawekezaji share
TKituo cha Uwekezaji Tanzania ni mahali pa kuanzia kwa mwekezaji mtarajiwa. Ni taasisi ya msingi ya Serikali yenye jukumu la kuratibu, kuhimiza, kukuza na kuwezesha uwekezaji . Kisheria idara na taasisi zote za Seriklali zimetakiwa zishirikiane kwa ukamilifu na TIC katika jitihada zake za kutimiza majukumu yake.
Kituo cha kuwezesha huduma zote mahali pamoja kinawasaidia wawekezaji (wa ndani na nje) alimradi wana miradi yenye thamani ya USD 100,000 (kwa Watanzania) na USD 300,000 (kwa wageni).
Kituo hikii kinawezesha kupta vivutio, usajili wa kampuni , upataji wa leseni za biashara, ulipaji kodi, upataji wa ardhi, vibali vya kazi na viza za mwekezaji.
Wawekezaji katika uchimbaji wa madini na mafuta wanapata leseni zao kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Miradi inayohitaji ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP) inaratibiwa na kuwezeshwa na TIC na Wizara ya Fedha.