Quienes somos
Makao makuu
Kituo cha UwekezajiMtaa wa Shaaban Robert
S.L. P 938
Dar es Salaam
Simu: +255(22)2116328-32
Fax: +255(22)2118253
information@tic.co.tz
Kanda ya Kaskazini
Meneja wa kanda ya kasksziniS.L. P 7735
Jengo la Mkoa
Moshi – Kilimanjaro
Simu: +255(27)2751066
Fax: +255(27)273316
northernzonal@tic.co.tz
Kanda ya Ziwa
Meneja wa kanda ya ZiwaS.L. P 638
Mtaa wa Kenyata
Mwanza
Simu: +255(28)2540871/2
Fax: +255(28)2540884
lakezone@tic.co.tz
Nyanda za juu Kusini
Meneja wa nyanda za juu KusiniS.L. P 1316
Karume Avenue , Jengo la NBC
Mbeya
Tel: +255(25)2504231
Fax: +255(285)250439
southernzone@tic.co.tz
The Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) imeanzishwa mwaka 1997 kwa Sheria ya Uwekezaji Tanzania kiwe “Taasisi kuu ya Serikali ya kuratibu, kuhimiza, kukuza na kuwezesha uwekezaji nchini Tanzania na kuishauri kuhusu sera ya uwekezaji na masuala yanayohusiana na uwekezaji”.
Taasisi hii inashughulika na uwekezaji wote wenye mtaji usiopungua USD 300,000 iwapo mmiliki ni mgeni au USD 100,000 iwapo mmiliki ni mwananchi. Shughuli za uwekezaji zinazohusu uchimbaji wa madini na petroli zitafuata utaratibu ulioidhinishwa kwenye sheria husika. Hata hivyo taasisi hii itasaidia wawekezaji wote kupata vibali, idhini nk. vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria nyingine ili kuanzisha na kuendesha uwekezaji nchini Tanzania.
Kazi za TIC ni pamoja na:
- Kuweka na kudumisha mazingira mazuri ya uwekezaji kwa sekta binafsi;;
- Kuishauri Serikali kuhusu masuala ya uwekezaji;
- Kuchochea uwekezaji wa ndani na wa nje;
- Kuwezesha wawekezaji wa ndani na wa nje;
- Kuchochea na kusaidia ukuaji Ujasiriamali Mdogo na wa Kati (SMEs) nchini Tanzania;
- Kutoa na kusambaza taarifa mpya kuhusu fursa za uwekezaji na vivutio vilivyopo kwa wawekezaji;
- Kufuatilia mazingira ya biashara nchini Tanzania na ukuaji wa Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Nje (FDI) nchini.
Shughuli za kila siku za TIC ni pamoja na:
- Kushughulikia kwa ukamilifu mahitaji ya mwekezaji;
- Kuchochea na kuwezesha maendeleo ya stadi za ujasiriamali na ukuaji wa wawekezaji wa ndani ikiwemo Ujasiriamali Mdogo na wa Kati (SME);
- Kuihudumia Kamati ya Taifa ya Uendeshaji Uwekezaji nchini (NISC);
- Uwezeshaji ukuaji wa SME na uhusiano na wabia wa miradi ya pamoja;
- Kufuatilia uingizaji wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni;
- Kuandaa mikutano ya uwekezaji ;
- Kutathmini wakati wote ushindani wa uwekezaji Tanzania;
- Kutangaza Tanzania kama mahali panapofaa kuwekeza;
- Kuhamasisha sera;
- •Kubadili utamaduni wa Serikali kwa njia ya semina za uhamasishaji.
Kama Mwezeshaji wa Kupata Taarifa za uwekezaji “Mahali Pamoja”, TIC:
- Inasaidia mwekezaji kupata vibali vyote , leseni na viza;
- Kutoa haki kwa mwekezaji zinazohusiana na ardhi;
- Kuwasaidia wawekezaji kukwamua vikwazo vya kiutawala na kisheria;
- Kutoa huduma ya “baada ya kuwekeza” kwa wawekezaji walioasajiliwa na TIC;